Sauti za Kuimba Community

Welcome to Sauti za Kuimba Community Forums.

NIMEKAA NINAJIULIZA

Posted by Kagori Kingori - Dec 15, 2019


NIMEKAA NINAJIULIZA 1.Nimekaa ninajiuliza, (pekee yangu) nimefanya nini kwa Mungu (Baba yangu), nimekaa ninajiuliza (pekee yangu) nimepokea bado kutoa x2 Bwana pokea chochote nikupacho (hata) ni kidogo ee Bwana kibariki x2 Uu nipe moyo wangu kwa shangwe kuu nimepokea bado kutoa x2 2.Sikia Bwana asemavyo (mwenzangu) kila kitu ninakijua (hesabu yake) hata nywele ninazijua, (hesabu yake) nimepokea bado kutoa x2 3.Nimekaa ninajiuliza (pekee yangu), mwili huu ni mwili wa nani (wa Mungu), nimekaa ninajiuliza (pekee yangu) nimepokea bado kutoa x2

NAKUJA MBELE ZAKO

Posted by Kagori Kingori - Dec 15, 2019


NAKUJA MBELE ZAKO 1.Nimekaa mimi najiuliza moyoni nitaendaje mbele za Bwana kwani Bwana amenilinda salama, amezibariki kazi zangu Mungu baba pokea nilicho nacho Nakuja mbele zako (Bwana) ninakuja na zawadi yangu ingawa ni kidogo sana Bwana uipokee x2 2.Ninatoa kwa moyo mkunjufu pokea hiki kidogo nilicho nacho, yote hayo ni kwaajili yako pokea, uzidi kunijalia mema, ninaleta mbele ya altare yako 3.Mkate na divai tunaleta pokea, ugeuze mwili pia damu hata fedha zetu za mifukoni twakupa yote ni mali yako pokea, tubariki tupokee mbele zako

NAJONGEA

Posted by Teddy Wambua - Dec 11, 2019


NAJONGEA KIITIKIO Naja mbele zako Bwana najongea kwenye altare (yako) (Bwana wangu) nikupokee wewe Bwana kwa mwili na damu Njoo kaa ndani yangu Bwana mimi nifarijike (ili) (Bwana wangu) niishi nawe Yesu uniongoze daima Sop-(Karibu Yesu mwokozi wangu,ukae ndani yangu,ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2 Alto-(Karibu Yesu,ukae ndani,ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2 Tenor-(Karibu Yesu mwokozi wangu,ukae ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2 Bass-(Karibu Yesu wangu ukae ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2 MASHAIRI 1.Bwana nishibishe na chakula hicho cha roho,unishinishe siku za maisha yangu yote 2.Nafsi yangu yakuonea kiu wewe Bwana,uninyweshe nisione kiu milele yote 3.Katu sikustahili kuijongea altare,unihurumie nipokee mwengi wa rehema 4.Niishi kiekaristia hadi nikate roho,mwisho nifufuke niishi nawe milele yote

Nitamuimbia Mungu

Posted by Teddy Wambua - Dec 11, 2019


Nitamuimbia Mungu UTANGULIZI Kama vile Daudi alivyomtukuza Mungu,akayavua mavazi yake ili amchezee, Ndivyo nami nitakavyomtukuza Mungu wangu,kwa sauti tamu nyororo yangu nikimsifu KIITIKIO All -Nitamuimbia Mungu wangu milele,nitampa sifa shangwe milele Sop/alto - Siku,wiki,miezi miaka,nafsi yangu itamsifu milele yote Tenor -Siku Bwana,wiki miezi miaka yote,nafsi yangu msifu milele yote Bass -Siku na wiki miezi miaka yote,nafsi yangu msifu milele yote MASHAIRI 1.Alinijua hata kabla nizaliwe (mimi),(na) ananiongoza kwa yote hadi leo,milele apewe sifa na utukufu 2.Ananilinda usiku pia mchana (mimi),(na) ananijalia hayo ninayohitaji,milele apewe sifa na utukufu 3.Kipaji cha uimbaji yeye kanipa (mimi),(na) nitakitumia vizuri kumsifu,milele apewe sifa na utukufu

TABASAMU LA UPENDO

Posted by Teddy Wambua - Dec 11, 2019


TABASAMU LA UPENDO Mashairi Sop/Alto 1.Ingawa ni mwepesi wa kusahau Bwana nifundishe upendo,maana wewe Mungu muumba wa vyote wewe mwenyewe upendo, Ukaniumba mimi kwa mfano wako kudhihirisha upendo, ukamtoa mwana wako wa pekee Yesu afe kwa ajili yangu, 2.Nijinyime anasa kukutumikia wewe huo ni upendo,neema rehema furaha faraja vyote nijaze kwa upendo, Kila nikikutafakari nikiwaza nikumbuke upendo,mawazo yangu (ya) daima yawe yamezingirwa na upendo, KIITIKIO Sop:(Bwana unipe upendo unijaze upendo,nami nihubiri upendo kwa walimwengu nasi Bwana,utubariki na tuweze kupendana daima tutabasamu tabasamu la upendo (wa)×2 wako. Alto:(we Bwana unijaze upendo,nihubiri kwao walimwengu nasi,we Bwana tubariki na tupendane,daima tutabasamu tabasamu la upendo)×2 wako. Tenor:(Bwana Mungu wangu nijaze upendo kama ulivyo nami nihubiri upendo kwa walimwengu upendo Bwana tubariki na tabasamu lako daima tutabasamu tabasamu la upendo (wa)×2 wako. Bass:(Bwana unipe upendo unijaze upendo nihubiri upendo kwa walimwengu nasi Bwana tubariki tuweze kupendana na tutabasamu tabasamu la upendo wako)×2. KIBWAGIZO Tenor:1.popote ninapoenda mataifa yakiri upendo wake :2.njia zote nipitazo zilindwe zikingwe nazo nguvu zake Sop:Bwana aliyejaa neema na upendo ae Alto:aliyejaa upendo ae Tenor:Bwana aliyejaa neema na upendo ae Bass:Bwana aliyejaa neema na upendo ae Alto:1.naam upendo wake Bwana nivumishe kwayo :2.naam na nguvu za shetani mwovu na zishindwe Sop:(nasi tutabasamu tabasamu la upendo)×2 wa Alto:(daima tutabasamu tabasamu la upendo)×2 Tenor:(daima tutabasamu tabasamu la upendo)×2 Bass:(tutabasamu tabasamu la upendo)×2 wako *Baada ya kibwagizo rudi kwenye kiitikio*