Sauti za Kuimba Community

Welcome to Sauti za Kuimba Community Forums.

Chombo cha amani

Posted by Lewis kaiser marube - Dec 31, 2018


MUNGU UNIFANYE CHOMBO CHA AMANI Music key;G major By;lewis k marube. Mungu unifanye mi niwe chombo,mi chombo cha amani yako,Mungu unifanye mi niwe chombo niweze kuhubiri neno,nishike mkono Mungu ,unikinge kwa mabawa yako ukeshaye kwa wazalendo tuhubiri injili wakenya*2 1)Tuna upendo tuna amani,ni faraja si tuna umoja, na Kenya yetu kwa wimbo wetu utufanye chombo cha amani 2)Tusipende matumbo yetu,tusahau si tuna wajibu, niwajibu wautenda kazi,kuhubiri injili kwa wote

How can I purchase online/download the songs

Posted by Evans Ochieng - Dec 01, 2018


Please guide me. 0723405253

shukrani

Posted by PAUL MUNGUTI - Oct 27, 2018


asante kwa hizi nyimbo na mwenye alianzisha hio wazo zimesaidia kwaya mingi sana Mungu awabariki wote

ASANTE BABA ASANTE

Posted by SAMWEL WACHIRA - Oct 25, 2018


Ninakushukuru Baba yangu nasema asante, umenitendea mengi makuu Baba asante x2 [Asante Baba asante, asante nashukuru kwa pendo la ajabu pokea sifa hizi)x2 1. Umenilisha mwili wako chakula chenye uzima, umeninywesha damu yako kinywaji chenye uzima(Jinsi gani nikushukuru Sina cha kukulipa wewe Lilobaki nikushukuru Asante ninashukuru) 2. Umenilinda mchana kutwa na usiku, wiki nzima, mwezi mzima hata mwaka (Jinsi… 3. Mema mengi wanijalia bila mimi kutarajia ingawa mimi ni mdhambi umenipenda bila mwisho(Jinsi… 4. Mvua nyingi zinanyesha, mimea nayo yasitawiMavuno mengi mashambani, chakula kingi manyumbani (msimu wa joto na baridi zapendeza, hizi zote ni Barakazako kwetu sisi) x2(Jinsi…

Umenichunguza - Ochieng' Odongo

Posted by Jude Maiyo - Oct 12, 2018


Wewe Bwana umenichunguza ukanifahamu nilivyo mimi X2 Nikiketi(Bwana) nikisimama(na nikisimama) wewe Bwana wanijua mimi X2 1. Niende wapi nikajifiche, nikautoroke uso wako Bwana, nikautoroke uso wako Bwana. 2. Ninapolala na kuamka, wewe Bwana wangu kweli wanijua, wewe Bwana wangu kweli wanijua 3. Maneno yangu pia matendo, na mawazo yangu Bwana wayajua, na mawazo yangu Bwana wayajua 4. Unyonge wangu na udhaifu, na kwa kutotimiza wajibu wangu, na kwa kutotimiza wajibu wangu 5. Maarifa yako ni ya ajabu, Bwana nakuomba ukaniongoze, Bwana nakuomba ukaniongoze