Sauti za Kuimba Community

Welcome to Sauti za Kuimba Community Forums.

2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China

Posted by Angela Pardie - Sep 29, 2018


China ni nchi ambamo joka kubwa jekundu hukaa, na ni mahali ambapo pamempinga na kumshutumu Mungu zaidi sana katika historia. China ni kama ngome ya mapepo na gereza linalodhibitiwa na shetani, lisilopenyeka na lisiloingilika. Zaidi ya hayo, utawala wa joka kubwa jekundu husimama ukilinda katika ngazi zote na umeanzisha ulinzi katika kila kaya. Matokeo yake, hakuna mahali pagumu zaidi ya hapa kueneza injili ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu. Wakati Chama cha Kikomunisti Cha China kiliposhika madaraka mwaka wa 1949, imani za kidini katika China bara zilizimwa kabisa na kupigwa marufuku. Mamilioni ya Wakristo walipitia mateso na fedheha hadharani, na kifungo. Makanisa yote yalifungwa kabisa na kufutiliwa mbali. Hata mikutano ya nyumbani ilipigwa marufuku. Iwapo mtu yeyote alibambwa akishiriki mkutano, angetiwa gerezani na hata angekatwa kichwa. Wakati huo, shughuli za kidini karibu zitoweke bila kupatikana. Ni idadi ndogo tu ya Wakristo iliendelea kuamini katika Mungu, lakini wangeweza tu kumwomba Mungu kimyakimya na kuimba nyimbo za sifa kwa Mungu katika mioyo yao, wakimwomba Mungu kufufua kanisa. Hatimaye, katika mwaka wa 1981, kanisa lilifufuka kwa dhati, na Roho Mtakatifu akaanza kazi kwa kiasi kikubwa katika China. Makanisa yakachipuka kama machipukizi ya mianzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua, na watu zaidi na zaidi wakaanza kuamini katika Mungu. Katika mwaka wa 1983, wakati uamshaji wa kanisa ulifika kilele chake, Chama cha Kikomunisti Cha China kikaanza duru mpya ya ukandamizaji wa kikatili. Mamilioni ya watu walikamatwa, wakawekwa kizuizini, na kuelimishwa kwa njia ya kazi. Utawala wa joka kubwa jekundu uliwaruhusu waumini katika Mungu kujiunga tu na Kanisa la Nafsi Tatu la Kizalendo (Three-Self Patriotic Church) lililoanzishwa na serikali. Serikali ya Chama cha Kikomunisti Cha China (CCP) lilianzisha Kanisa la Nafsi Tatu la Kizalendo (Three-Self Patriotic Church) katika jaribio la kuzima kanisa la siri la nyumbani na kuwaleta wale waumini wa Bwana imara chini ya utawala wa serikali. Iliamini kwamba hii ilikuwa njia pekee ya kufikia lengo lake la kupiga marufuku imani na kugeuza China kuwa nchi isiyokuwa na Mungu. Lakini Roho Mtakatifu aliendelea kufanya kazi nyingi katika kanisa la nyumbani na katika wale ambao kweli waliamini katika Mungu, ambao serikali ya CCP ilishindwa kuwakomesha. Wakati huo, katika kanisa la nyumbani ambapo Roho Mtakatifu alifanya kazi, Kristo wa siku za mwisho kwa siri Alionekana Akifanya kazi, na kuanza kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Terms of use

Have You Been Rapturned? | "Kutamani Sana" | Swahili Christian Movie

Posted by Angela Pardie - Sep 26, 2018


Miaka elfu mbili iliyopita, BwanaYesu aliwaahidi wafuasi Wake: "Naenda kuwatayarishia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia" (Yohana 14:2-3). Kwa sababu ya hili, vizazi vya waumini vimeendelea kujawa na tumaini na kushikilia maombi kwa ajili ya kutimizwa kwa ahadi ya Bwana, na kutumaini na kuomba kwamba wanyakuliwe hadi kwenye mbingu ili kukutana na Bwana na kuingia katika ufalme wa mbinguni wakati Bwana atakapokuja. Huu pia unamfafanua mhusika mkuu wa filamu, Chen Xiangguang. Ni mtafutaji mwenye shauku kubwa, anaieneza injili, na kumshuhudia Bwana ili kukaribisha kurudi kwa Bwana. Licha ya kuachishwa kazi shuleni na kushindwa kupata huruma kutoka kwa familia yake, katu hakati tamaa moyoni mwake. Siku moja akiwa kwenye kikao, Chen Xiangguang anakamatwa na kutiwa gerezani na serikali ya Kikomunisti ya Kichina. Kupitia kwa utawala na mipangilio ya ajabu ya Mungu, anakutana na Zhao Zhiming, Mkristo kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Zhao Zhiming anamtolea ushuhuda kuhusu kuonekana kwa Mungu na kazi katika siku za mwisho na kumtatulia miaka yake ya mawazo na fikira kwa kutumaini na kuomba kwa ajili ya kurudi kwa Bwana. Baada ya kutoka gerezani, Chen Xiangguang anawaongoza kaka na dada zake katika kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kila mtu hatimaye anafahamu maana ya kunyakuliwa hadi kwenye ufalme wa mbinguni, haijalishi kama ufalme umo hasa ulimwenguni au mbinguni, na namna ambavyo watu wanafaa kukaribisha kurudi kwa Bwana … Terms of use

Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Posted by Angela Pardie - Sep 22, 2018


Mwenyezi Mungu alivyosema, "Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji wingi wa neema, ustahimili usio na mwisho na uvumilivu, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu waliona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya dhambi ya binadamu,Yesu. Na walijua kwamba ni Mungu tu ndiye Anaweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na waliona tu huruma wa Yesu na fadhili Zake. Hii ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Hivyo kabla ya kukombolewa, walilazimika kufurahia neema nyingi ambayo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia kwa ustahimili wa Yesu na uvumilivu."

Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu

Posted by Angela Pardie - Sep 17, 2018


Wimbo Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu I Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda, uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme. Maneno Yako yamenitakasa, yakanifanya nianze kuishi maisha ya furaha. Moyoni mwangu nahisi, kwa kweli, ni upendo Wako mkuu. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Maneno Yako yote ni ukweli. Unastahili upendo wa binadamu. Ee Mungu! Ukipuuza uasi wangu wa zamani, Unanijali na kufanya kazi kuniokoa. Unaniongoza katika njia ya kweli, Ukitazama kila wakati katika upande wangu, natarajia tu nitakua na kuwa mtu mpya. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Nitafuatilia kukupenda Wewe, mwaminifu kwa wajibu ili kukufurahisha Wewe. II Ee Mwenyezi Mungu?, maneno Yako yamenitakasa. Neema Yako ya wokovu sitasahu kamwe. Nitakupenda Wewe maisha yangu yote, nikiuridhisha moyo Wako. Uliacha mengi sana ili kuniokoa, na sitakukosea Wewe kamwe. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Nitakupenda Wewe maisha yangu yote, mwaminifu katika wajibu, katika wajibu. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Nitakupenda Wewe maisha yangu yote, mwaminifu katika wajibu, katika wajibu.   kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya Nyimbo za Uzoefu wa Maisha | INJILI YA KUSHUKA KWA UFALME https://sw.kingdomsalvation.org/i-will-be-loyal-in-duty.html

EKASH MASS

Posted by MBONDO BERNARD - Jun 03, 2018


Ekash mass lyrics MASS BY MBONDO BERNARD MWANIA TEL: +254701943386 EMAIL: bernajemo@gmail.com ADDRESS: 68 – 90119 Matuu (KENYA) Utuhurumie S/A Bwana( ee )bwana bwana tuhurumie T/B (ee bwana) All tumekosa bwana tuhurumie *2 S/A kristu (ee) kristu kristu tuhurumie T/B (ee bwana) All tumekosa bwana tuhurumie S/A Bwana ( ee )bwana bwana tuhurumie T/B (ee bwana) All tumekosa bwana tuhurumie *2 Utukufu Utukufu juu kwa mungu – na Amani kote duniani Kwao watu wa mapenzi mema Tunakusifu baba twakuheshimu baba twakuabudu baba twakutukuza *2 Twakushukuru mungu mfalme – twakushukuru kwau tukufu wako Mfalme wa mbingu ndiwe baba yetu Mwokozi wetu yesu kristu – mwana pekee mwana wake baba Uliye mwaanakondoo wa mungu Uondoaye dhambi zote – uondoaye dhambi za dunia Maombi yetu yapokee kwako Unayeketi kuume kwake – unayeketi kuume kwa baba Sikiza sala zetu wana wako Pekee yako ndiwe bwana – pekee yako mkombozi mkuu Pekee yaako u’mtakatifu Na kwa pamoja naye roho – na ndani yake baba watukuzwa Ewe yesu milele amina Aleluyia Aleluyia aleluyia aleluyia aleluyia aleluyia*2 Nasadiki S Nasadiki kwa mungu mmoja All Nasadiki kweli S/A Ndiye baba yetu mwenyezi All Ninasadiki S Mwumba mbingu pia dunia All nasadiki kweli S/A Nasadiki kwa yesu kristu All Ninasadiki Nasadi (ninasadiki) nasadi (ninasadiki) nasadiki mimi kweli ninasadiki *2 2. Mwumba mbingu pia dunia – Mwenye kuzaliwa kwa baba – Akapata mwili kwa roho – Kazaliwa naye bikira – 3. Kisha yeye kasulubiwa – Kwa mamlaka yake pilato – Kwa ajili yetu kateswa – Ye akafa na akazikwa – 4. Kafufuka katika wafu – Akapaa juu mbinguni – Ameketi kuume kwake – Mungu baba yetu mwenyezi – 5. Ndipo atakapotokea – Ili awahukumu wote – Kwake Roho mtakatifu – Kwa kanisa la katoliki – 6. Ushirika wa watakatifu – Ondoleo la dhambi zetu – Nangojea ufufuko wa miili – Na uzima wa milele – Maombi Ee bwana sikia kilio chetu – sisi (bwana) tunakulilia jangwani Mtakatifu Mtakatifu (mmh) mtakatifu (ee) bwana mungu wa majeshi *2 Mbingu na dunia mbingu na dunia zimejaa utukufu wako *2 Hosanna( hosanna) hosanna (hosanna) hosanna, juu mbinguni *2 Mbarikiwa (mmh) mbarikiwa (ni) yeye ajaye kwa jina la bwana *2 Hosanna ( hosanna) hosanna (hosanna) hosanna, juu mbinguni *2 Fumbo la Imani Twakiri kristu alikufa (kristu) akafufuka {kristu atakuja kwetu tena} *2 Amina Aamina aamina aamina aamina aamina *2 MWANAKONDOO Ee mwanakondoo wa mungu – mwana wake baba ee mwana ee mwana tuhurumie Ee mwanakondoo wa mungu – mwana wake baba ee mwana ee mwana tuhurumie Ee mwanakondoo wa mungu – mwana wake baba ee mwana ee mwana tujalie Amani