Sauti za Kuimba Community

Welcome to Sauti za Kuimba Community Forums.

SIKIA KILIO CHETU by mbondo bernard

Posted by MBONDO BERNARD - Apr 22, 2017


[Ee Bwana sikia kilio chetu sisi tunakulilia jangwani] *2

KARAMU YA BWANA by Mbondo Bernard

Posted by MBONDO BERNARD - Apr 21, 2017


KIITIKIO Twendeni wote (kwa bwana) mezani pake (tukale) tujongeeni kwa karamu ya bwana *2 MASHAIRI. 1. Tule mwili na tunywe damu yake,atushibishe,tupate nguvu za roho Alaye mwili na kuinywa damu,ana uzima,ana uzima wa milele. 2. Wateule twende wenye mizigo,tumpelekee,atatupumzisha. Aponya magonjwa ye' ni tabibu,ole wenu,msitao kujongea 3. Shangwe kuu mlimani bwana,heri yupe anashiriki karamu Anageuza mkate divai,mwili na damu,tujongee altare 4. Katika safari hii ya mbinguni,kunayo njia, naye rubani ni yesu Aendesha tu wenye kuyatii,mafundisho,waombao na kutubu. 5. Tumpokee tukiwa duniani,adumu kwetu,nasi kwake tutaishi. Tarumbeta itakapopulizwa,atupokee,atupeleke kwa baba

Nota za Nyimbo

Posted by Wamalwa Wanyama Silvanos - Dec 23, 2016


Nawashukuru wote wanaofanikisha kuwepo kwa maneno ya nyimbo katika tovuti hii. Pia nashukuru kwa maendeleo tunayoyashuhudia ya kuwepo njia ya kufikia nota za nyimbo. Mola awabariki sana kwa hili ili tuzidi kuieneza Injili ya Yesu kwa njia ya nyimbo. Basi naomba haswa nota za nyimbo za kwaya ya Chuo Kikuu Cha Nairobi (St. Pauls UON student's choir) kwa maana nyimbo zenyewe tamu kweli kweli lakini mie kama mkufunzi wa muziki nashindwa kuziimbisha katika kwaya yangu kwa maana sina uhakika wa nota. Nitashukuru.

REQUEST

Posted by MUSEKURA - Mar 30, 2016


I am grateful for the Apostolate you're doing in this respect. Music is a great treasure for the Church in the edification of her members. Keep it up!!!!! My email is musekuraanthony@gmail.com Send me those music pieces so that i go to teach them in my Pastoral Work.. Asante...

Nitayainua macho yangu

Posted by Dan - Feb 11, 2016


Nitayainua macho yangu niitazame milima msaada wangu utatoka wapi? msaada wangu u katika BWANA,Aliyezifanya mbingu na nchi,Hatasinzia wala hatalala,Atanilinda na mabaya yote na nafsi yangu,Maisha yangu na familia yangu sea nayakabidhi kwako mola wangu tangu sasa na hata milele.