Nota za Nyimbo - Sauti za Kuimba Community

Posted by Wamalwa Wanyama Silvanos - Dec 23, 2016


Nawashukuru wote wanaofanikisha kuwepo kwa maneno ya nyimbo katika tovuti hii. Pia nashukuru kwa maendeleo tunayoyashuhudia ya kuwepo njia ya kufikia nota za nyimbo. Mola awabariki sana kwa hili ili tuzidi kuieneza Injili ya Yesu kwa njia ya nyimbo. Basi naomba haswa nota za nyimbo za kwaya ya Chuo Kikuu Cha Nairobi (St. Pauls UON student's choir) kwa maana nyimbo zenyewe tamu kweli kweli lakini mie kama mkufunzi wa muziki nashindwa kuziimbisha katika kwaya yangu kwa maana sina uhakika wa nota. Nitashukuru.