KARAMU YA BWANA by Mbondo Bernard - Sauti za Kuimba Community

Posted by MBONDO BERNARD - Apr 21, 2017


KIITIKIO Twendeni wote (kwa bwana) mezani pake (tukale) tujongeeni kwa karamu ya bwana *2 MASHAIRI. 1. Tule mwili na tunywe damu yake,atushibishe,tupate nguvu za roho Alaye mwili na kuinywa damu,ana uzima,ana uzima wa milele. 2. Wateule twende wenye mizigo,tumpelekee,atatupumzisha. Aponya magonjwa ye' ni tabibu,ole wenu,msitao kujongea 3. Shangwe kuu mlimani bwana,heri yupe anashiriki karamu Anageuza mkate divai,mwili na damu,tujongee altare 4. Katika safari hii ya mbinguni,kunayo njia, naye rubani ni yesu Aendesha tu wenye kuyatii,mafundisho,waombao na kutubu. 5. Tumpokee tukiwa duniani,adumu kwetu,nasi kwake tutaishi. Tarumbeta itakapopulizwa,atupokee,atupeleke kwa baba