EKASH MASS - Sauti za Kuimba Community

Posted by MBONDO BERNARD - Jun 03, 2018


Ekash mass lyrics MASS BY MBONDO BERNARD MWANIA TEL: +254701943386 EMAIL: bernajemo@gmail.com ADDRESS: 68 – 90119 Matuu (KENYA) Utuhurumie S/A Bwana( ee )bwana bwana tuhurumie T/B (ee bwana) All tumekosa bwana tuhurumie *2 S/A kristu (ee) kristu kristu tuhurumie T/B (ee bwana) All tumekosa bwana tuhurumie S/A Bwana ( ee )bwana bwana tuhurumie T/B (ee bwana) All tumekosa bwana tuhurumie *2 Utukufu Utukufu juu kwa mungu – na Amani kote duniani Kwao watu wa mapenzi mema Tunakusifu baba twakuheshimu baba twakuabudu baba twakutukuza *2 Twakushukuru mungu mfalme – twakushukuru kwau tukufu wako Mfalme wa mbingu ndiwe baba yetu Mwokozi wetu yesu kristu – mwana pekee mwana wake baba Uliye mwaanakondoo wa mungu Uondoaye dhambi zote – uondoaye dhambi za dunia Maombi yetu yapokee kwako Unayeketi kuume kwake – unayeketi kuume kwa baba Sikiza sala zetu wana wako Pekee yako ndiwe bwana – pekee yako mkombozi mkuu Pekee yaako u’mtakatifu Na kwa pamoja naye roho – na ndani yake baba watukuzwa Ewe yesu milele amina Aleluyia Aleluyia aleluyia aleluyia aleluyia aleluyia*2 Nasadiki S Nasadiki kwa mungu mmoja All Nasadiki kweli S/A Ndiye baba yetu mwenyezi All Ninasadiki S Mwumba mbingu pia dunia All nasadiki kweli S/A Nasadiki kwa yesu kristu All Ninasadiki Nasadi (ninasadiki) nasadi (ninasadiki) nasadiki mimi kweli ninasadiki *2 2. Mwumba mbingu pia dunia – Mwenye kuzaliwa kwa baba – Akapata mwili kwa roho – Kazaliwa naye bikira – 3. Kisha yeye kasulubiwa – Kwa mamlaka yake pilato – Kwa ajili yetu kateswa – Ye akafa na akazikwa – 4. Kafufuka katika wafu – Akapaa juu mbinguni – Ameketi kuume kwake – Mungu baba yetu mwenyezi – 5. Ndipo atakapotokea – Ili awahukumu wote – Kwake Roho mtakatifu – Kwa kanisa la katoliki – 6. Ushirika wa watakatifu – Ondoleo la dhambi zetu – Nangojea ufufuko wa miili – Na uzima wa milele – Maombi Ee bwana sikia kilio chetu – sisi (bwana) tunakulilia jangwani Mtakatifu Mtakatifu (mmh) mtakatifu (ee) bwana mungu wa majeshi *2 Mbingu na dunia mbingu na dunia zimejaa utukufu wako *2 Hosanna( hosanna) hosanna (hosanna) hosanna, juu mbinguni *2 Mbarikiwa (mmh) mbarikiwa (ni) yeye ajaye kwa jina la bwana *2 Hosanna ( hosanna) hosanna (hosanna) hosanna, juu mbinguni *2 Fumbo la Imani Twakiri kristu alikufa (kristu) akafufuka {kristu atakuja kwetu tena} *2 Amina Aamina aamina aamina aamina aamina *2 MWANAKONDOO Ee mwanakondoo wa mungu – mwana wake baba ee mwana ee mwana tuhurumie Ee mwanakondoo wa mungu – mwana wake baba ee mwana ee mwana tuhurumie Ee mwanakondoo wa mungu – mwana wake baba ee mwana ee mwana tujalie Amani