{ Acheni mimi, nimuimbie Muumba wangu,
Aliyeniumba, mimi kiumbe mwenye akili } *2
Aliyenipa uwezo wa kusimama hapa
Tangu tumboni mwa mama amenipa uhai
Juzi jana leo nimeamka kesho ajua yeye
Maisha yangu ayapa maziwa ni kama mtoto
{ Acheni mimi, nizitamke sifa za Mungu wangu
Na sitachoka, kumuimbia mimi ningali hai } *2
- [ b ] Nalala jioni na kuamka pia nazo nguvu,
Ninafanya kazi na kujipatia riziki zangu
- Amenipatia akili yangu na wangu ubunifu,
Shuleni kazini ninayoyafanya hayana pungufu,
- Mara nyingi sana ninajiuliza nitampa nini,
Kwani Bwana amenitendea mengi bila ya kwa nini
- Ninapokuwa nazo shida nyingi hunipa tulizo,
Kwake kila mara watu wote hupata burudiko.
|
|
|