Alfajiri ya Kupendeza

Alfajiri ya Kupendeza
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumTazameni Miujiza (Vol 2)
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerJ. C. Shomaly
Views43,209

Alfajiri ya Kupendeza Lyrics

  1. [ b ] Alfajiri ya kupendeza, ni siku njema siku yenye baraka,
    [ w ] Jua limekwishachomoza, laamsha wote waliolala
    Ndege nao wanalialia kumshukuru Muumba ( njooni )
    { Njooni baba, mama na watoto
    Njoni wote mbele za Bwana
    Tumtolee shukrani zetu, kwa kutoa sadaka } *2

  2. [ s ] Ndege wanamshukuru, kwa sauti za kupendeza
    Na sisi tumshukuru, kwa zawadi alizotupa (njooni)
  3. Wanyama pia na mimea, vyote vimeumbwa na Mungu
    Vitu vyote vya duniani, vyapaswa kumshukuru Mungu (njooni)
  4. Kaiumba dunia hii, kaweka giza pia mwanga
    Mchana tufanyeni kazi, usiku na tupumzike (njooni)