Alhamisi Kuu Lyrics

ALHAMISI KUU

@ (traditional)

 1. Alhamisi kuu Yesu alituwekea
  Ekaristia takatifu, chakula cha roho

  Tuimbe - tuimbe,
  Tumshukuru - tumshukuru Yesu, mkombozi wetu
  Tuimbe - tuimbe,
  Tumshukuru - tumshukuru Yesu, sadaka yetu

 2. Yesu alishika mkate akaubariki
  Akawapa wafuasi, ndio mwili wangu
 3. Na kikombe cha divai akakibariki
  Akasema, nyweni nyote, ndiyo damu yangu
 4. Yesu aliwapa amri wanafunzi wake
  Fanyeni hivi daima kwa kunikumbuka
 5. Kisha Yesu akaenda apate kuteswa
  Akafuta dhambi zetu msalabani juu
 6. Yesu anatutolea mwili na damuye
  Naye Baba wa mbinguni anatubariki
Alhamisi Kuu
COMPOSER(traditional)
CATEGORYAlhamisi Kuu
MUSIC KEYA Flat Major
TIME SIGNATURE4
4


Wimbo huu unaweza kuimbwa Siku ya Alhamisi Kuu au wakati wa Komunyo
 • Comments