Amezaliwa Masiya wetu

Amezaliwa Masiya wetu
Performed by-
CategoryNoeli (Christmas Carols)
Views6,936

Amezaliwa Masiya wetu Lyrics

  1. Amezaliwa Masiha wetu, hoyee hoye hoye
    Mwana wa Mungu mkombozi wetu, hoyee hoye hoye
    Leo kazaliwa naye Maria na amelazwa
    kwenye hori la wanyama, twende tukamwone
    Amekuja kwetu mwana wa Mungu kuzichukua
    dhambi zetu wanadamu, mkombozi wetu
    { Tumsujudie Bwana Mungu, kwa vigelegele
    Tucheze ngoma na kayamba tupige makofi } *2

  2. Amelala manyasini, twendeni tukamwone,
    Tukamsalimie Mkombozi wetu
    Kwa zawadi zetu za dhahabu uvumba na manemane
  3. Wachungaji waondoka, waenda Bethlehemu,
    Wakamsujudie Bwana Mkombozi,
    Wafurahi naye pamoja na Maria naye Yusufu
  4. Malaika wamefika wengi na wa mbinguni
    Tukajiunge nao tuimbe pamoja utukufu uwe
    Kwa Mungu juu amani kwa watu wenye mapenzi mema
  5. Tumpokee mkombozi Masiha amekuja
    Ewe mtoto Yesu ishi ndani yetu, tuangaze sisi,
    Kwa mwanga wako mwanga wa Mbinguni.