Bwana Unaweza Lyrics

BWANA UNAWEZA

Vipofu, viziwi, na wakoma wakapona
Makahaba wakaepuka kifo cha mawe
Wenye harusi wakajaliwa divai
Lazaro akafufuka siku ya tatu*
Nimekuita kwa hofu siku nyingi sana
Nimekulilia ili nisaidike
Unaweza unaweza Bwana,
Unaweza unaweza sana
Nitazame nitazame upya,
Nitazame kwa huruma yako

 1. Dhambi zangu zimegeuka mzigo kwangu
  Zinanizuia kuona hurumayo
  Unaweza unaweza Bwana
 2. Lakini niende wapi zaidi ya kwako
  Tena wewe una huruma ya milele
  Unaweza unaweza Bwana
 3. Nimekulilia siku nyingi nimeomba
  Shida zangu zinazidi kunilemea
  Unaweza unaweza Bwana
Bwana Unaweza
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMNakaza Mwendo (Vol 19-20)
CATEGORYTafakari
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania


* tatu - New versions sing:
Lazaro akafufuka siku ya nne
 • Comments