Bwana Unayoyatenda Lyrics

BWANA UNAYOYATENDA

@ J. C. Shomaly

{ Bwana unayoyatenda kwangu mimi ni huruma ya kweli
(ya kweli) sitakuwa na fadhila nisipokiri haya } *2
{ Kuniumba, bila ya kukwambia, akili yangu tofauti sana
Ninalala pia ninaamka tazama niko hai } *2

 1. Uhai nilio nao, sijanunua lolote,
  Bwana nashukuru sana ninasema asante
 2. Marafiki umenipa, maisha ya kupendeza,
  Bwana nashukuru sana ninasema asante
 3. Umenipa na watoto, yote sikutarajia,
  Bwana nashukuru sana ninasema asante
 4. Yote umetenda kwangu, bila mimi kuwa mwema
  Bwana nashukuru sana ninasema asante
Bwana Unayoyatenda
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMMbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments