Dhihirisha Fadhili Lyrics

DHIHIRISHA FADHILI

@ Bernard Mukasa

Dhirisha fadhili fadhili zako za ajabu
wewe uwaokoaye wanaokukimbilia
Wasinione wasio haki, wananionea
Adui za roho yangu wanaonizunguka
{ Bali mimi bali mimi niutazame uso
wako katika haki
Niamkapo nishibishwe kwa sura yako } *2

 1. Wamenishtaki kwa makosa yao wenyewe,
  Wakanihukumu kwa madhambi waliyotenda
  Wamekunywa damu yangu waonekane wema
  mbele ya watu
 2. Ushike kigao ushike ngao usimame
  Bwana utete nami
Dhihirisha Fadhili
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIR
CATEGORYZaburi
REFPs. 17
 • Comments