Tembea Nami Bwana

Tembea Nami Bwana
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumKidole Juu (Vol 23)
CategoryTafakari
ComposerC. A. L. Ndomelo
Views8,429

Tembea Nami Bwana Lyrics

  1. {Ee Bwana Mungu wangu
    Tembea nami usiniache kwenye dunia (hiyo)
    Ya machafuko } *2

    Nikianguka, Bwana, uniinue Bwana
    Nikiteleza, Bwana, unishike mkono
    Uniepushe na maadui wa roho yangu
    Uniepushe na maadui wa roho yangu

  2. Tazama ninaishi kwa mashaka na hofu kubwa
    (Kwani) Baadhi ya wanadamu wenzangu wamegeuka
    Kuwa ni maadui zangu,
    Wananiwinda wanikamate wavinyokoe viungo,
    Eti wajipatie mali.
  3. Tazama ninaishi kwa mashaka na hofu kubwa
    (Kwani) Baadhi ya waathirika wenzangu wamekamatwa
    Bwana na wameshauawa,
    Wamewakata vichwa na mikono, na miguu yao Bwana,
    Eti wajipatie mali
  4. Tazama sisi wanao wakiwa twakimbilia (kwako)
    (Kwako) twazikabidhi roho zetu mikononi mwako
    Maana ni wewe kimbilio
    Usituachie adui zako watutie mikononi
    Bwana utushike mkono