Harusi Kidededede Lyrics

HARUSI KIDEDEDEDE

@ Alfred Ossonga

 1. { Bwana harusi na bibi harusi, leo mmefunga ndoa ya maisha,
  Kaeni kwa amani kidededede } * 2

  Upendo wenu umedhihirika
  Uyani kwenu bamba ishini tototo
  Uzuri wenu hauna kifani
  Uyani kwenu bamba ishini tototo
  Na nyumba yenu imebarikiwa
  Uyani kwenu bamba ishini tototo ooo

 2. Jitulize mjisikie sukari, siku ya leo ni yenu,
  Furahini, mmepambwa maua mnapendeza
 3. Bwana arusi kwanza wachangamka, bibi arusi chachawa,
  Chezacheza, penzi lenu leo limekamilika
 4. Mapenzi yenu yote yatasitawi, hakika yatasitawi,
  Yatamea, kama ule mwerezi wa Lebanoni
 5. Baraka zake Mungu ziwashukie, kaeni pasipo shida,
  Siku zote nyumba yenu iwe hekalu la Mungu.
Harusi Kidededede
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Anthoney Malindi
ALBUMMalindi Kuna Nini
CATEGORYHarusi
 • Comments