Hatuteteleki

Hatuteteleki
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly
Views3,232

Hatuteteleki Lyrics

  1. { Hatuteteleki na wala hatubabaishwi,
    Mioyoni mwetu hakuna cha kutusuasua
    Kwa kuwa tunaye mwenyezi Mungu mwenye haki } *2

    { Ukiwa na imani na Mungu -
    Hautaaibishwa, hautatishwatishwa,
    hautadhamiria dhambi
    Kama ni maisha ya dunia -
    Utakula na kunywa, utavaa vizuri,
    Utapata hata na watoto,
    Tena wenye tabia njema na elimu bora } *2

  2. Ndani yake yeye ni utamu, shida haijui watu wake,
    Kweli Mungu ni mwema
  3. Afya njema aliumba yeye, utajiri aujua yeye,
    Kweli Mungu ni mwema
  4. Wa dunia wakikusimanga, Mungu atafanya unenepe
    Kweli Mungu ni mwema
  5. Kazi zako watakupangia, Hata sio kwa idhini yako
    Mungu awasamehe.