Hebu Jiulize Lyrics

HEBU JIULIZE

@ E. A. Minja

{Hebu jiulize lingetolewa tangazo leo
Ya kwamba kila apumuaye
na ailipie pumzi avutayo } *2
Ni nani angejificha asilipe kodi,
Ni nani angesema yeye ni masikini,
Ni nani angekwepa kwani yeye ni tajiri
Ni nani angekuwa kweli mtu wa kiburi
Ni nani angekwepa kweli kulipia kodi (nasema)
Ni nani angependa kunyang’anywa uhai wake * 2

 1. Tazama sasa majirani zako wote,
  Hakuna unayeongea naye
  Kwani unawadharau
  kwa kuwa wao hawana fedha kama zako
  Hebu tazama baadhi ya ndugu zako,
  Hupendi hata kuwaona kwako
  Unawakana kwa kuwa, wao ni maskini,
  tena unawaona ni wachafu.
 2. Kwa nini hivyo, biashara zako,
  wewe unawaajiri wafanya kazi
  Tena ni wachapa kazi na mwisho wa mwezi,
  huwafichia eti wameiba
  Hebu tazama wapoteza fedha nyingi,
  unapokuwa baa na marafiki
  Kwa ajili tu ya anasa, na kuwasaidia,
  maskini kwako ni hasara
 3. Jitafakari, fungua na legeza moyo wako
  kwa kuwajali wasiojiweza
  Na wenye shida mbalimbali, na sio kuegeza
  Hazina ya moyowe kwa shetani.
Hebu Jiulize
COMPOSERE. A. Minja
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMchanganyo
CATEGORYTafakari
 • Comments