Hii Ndiyo Siku Lyrics

HII NDIYO SIKU

Hii ndiyo siku, aloifanya Bwana *2
Tuishangilie, na kuifurahiya *2
{Tupige makofi na vigelegele
Sote turuke juu tumshukuru Mungu } *2

 1. Ndiwe Mungu wangu nami nitakushukuru
  Ndiwe Mungu wangu nami nitakutukuza
  Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
  Kwa mema yote Bwana uliyonijalia
 2. Nifungulieni malango ya haki,
  Nitaingia mimi na kumshukuru Mungu
  Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
  Kwa mema yote Bwana uliyonijalia
 3. Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa
  Mkono wa Bwana hutenda makuu
  Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
  Kwa mema yote Bwana uliyonijalia
 4. Mshukuruni Bwana kwa kuwa yeye ni mwema
  Kwa maana fadhili zake ni za milele
  Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
  Kwa mema yote Bwana uliyonijalia
Hii Ndiyo Siku
CHOIROur Lady of Fatima Kongowea
ALBUMKila Mwenye Pumzi (vol 4)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments