Isemavyo Torati Lyrics

ISEMAVYO TORATI

@ J. C. Shomaly

{ Isemavyo torati ya kale, jicho kwa jicho, jino kwa jino
Mkuki kwa mkuki, hiyo silaha ya mababu } *2
{ Lakini mimi, ninawaambia, nawaambia,
Msilipize kisasi kwa mambo haya } *2

Akupigaye shavu lako moja, mgeuzie na la pili
Akunyang'anyaye na joho lako -
Mpe pia kanzu yako, utayashinda majaribu.

 1. Ndugu nawaambia nyinyi, jifunzeni kusameheana
  Acheni chuki ubinafsi, hazisaidii kwa vyovyote.
  Ukikosewa samehe, sababu hata wewe wakosea
  Mungu asingesamehe, wewe na mimi tungekuwa wapi
 2. Wewe unayemchukia huyu, huyu ameumbwa naye Mungu
  Kumbuka wote sisi twapita, hakuna aishiye milele
  Wamuua huyu na wewe, utakufa siku moja kama yeye
  Utajibu nini kwa Mungu, kuifanya kazi yake bila ruhusa
 3. Riziki aitoa Mungu, acha wivu pia masengenyo
  Mwenzako amepata kwa jasho, fanya bidii ufanikiwe
  Wamwonea wivu kwa nini, na kuanza kuharibu na kuiba
  Utajibu nini kwa Mungu, kuharibu nchi yake aliyoumba
Isemavyo Torati
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMMshike Mshike (Vol 5)
CATEGORYTafakari
REFMt. 5
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE3
8
 • Comments