Jipe Moyo

Jipe Moyo
Performed by-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Views13,466

Jipe Moyo Lyrics

  1. Jipe moyo Bwana yuko nawe, (tena)
    Hakuachi kamwe kwani yeye akupenda
    Hata shida zikikuandama (ndugu)
    Umtegemee, Yesu atakuongoza

  2. Njia imejaa giza na umande,
    Huku watembea bila hata nuru wasi wasi
    Hofu yakujaa woga watawala
    Wasimama wima hujui pa kwenda
    Ushujaa watoka wabaki upweke,
    Bali yu pamoja na wewe
  3. Ndugu watoweka wakuacha pweke,
    Hata marafiki uliothamini watoroka
    Hofu yakujaa woga watawala
    Wasimama wima hujui pa kwenda
    Ushujaa watoka wabaki upweke,
    Bali yu pamoja na wewe
  4. Kila utendacho, hakiwezekani,
    Wajaribu sana kufaulu wala hauwezi
    Hofu yakujaa woga watawala
    Wasimama wima hujui pa kwenda
    Ushujaa watoka wabaki upweke,
    Bali yu pamoja na wewe