Kama Kunguru Lyrics

KAMA KUNGURU

@ J. C. Shomaly

{ Kama kunguru arukapo juu ya jalala kubwa
Akitafuta mizoga na wadudu
Alishibishe tumbo lake } *2

{ Ndivyo moyo wake mtu asiyempenda Mungu
Utakuwa wa kubabaika na kuhangaika
Hatakuwa na amani,
Atakuwa kama kunguru tu, kama kunguru tu,
Awindaye toka macheo ya jua hata yapata mawio
Na tumbo lake bado ni tupu } *2

 1. Moyo wako ndugu mbona waubabaisha,
  Kutwa kucha wewe umemsahau Mungu
  Dunia ina mambo yake - tena yanapita
 2. Kama una kiu na tamaa za dunia
  Zina mwisho wake kwanza mtafute Mungu
  Mungu alishapanga yako - hivyo umuombe
Kama Kunguru
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYTafakari
 • Comments