Kila Kunapokucha Lyrics

KILA KUNAPOKUCHA

{ Kila kunapokucha, ndugu zangu mimi
Wananikwepa na kunikimbia
Majirani zangu wanatazamana bila kunitamkia neno
Ewe Muumba wangu najiuliza na kujitafakari mimi
Au nimekuwa na sura ya simba,
Au nimekuwa na sura ya chui, hata ninatisha } *2

 1. Ninapokaa chini na kutafakari mwenendo wangu
  Kwani uko vipi mimi niliupenda,
  Japo magumu mimi niliyapata,
  Nilivaa sura ya kifalme pasipo kuwa na utu
 2. Nikiupekua pekua moyo wangu unanitisha
  Ni huo tena kwa kudhamiria
  Kwa kauli toka kwa ulimi wangu
  Nilifanana na jitu baya tena limezalo watu
 3. Hakuna adui hakuna rafiki kwangu wote sawa
  Hakuna mwema katika moyo wangu
  Wala rafiki katika roho yangu
  Nilijifananisha na chui tena chui mwenye njaa
Kila Kunapokucha
CATEGORYTafakari
SOURCEMwanza
 • Comments