Mataifa ya Ulimwengu

Mataifa ya Ulimwengu
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerJ. C. Shomaly
Views12,594

Mataifa ya Ulimwengu Lyrics

  1. { Mataifa yote ya ulimwengu
    Yatakusujudia ee Mungu (Mungu Baba) } *2
    { Mema uliyonitendea Mungu wangu ninashukuru
    Jana leo nimeamka kesho sijui itakuwa vipi
    Ninashukuru Mungu wangu leo
    Na nyimbo nzuri ninaimba ili kesho nayo niwe salama
    Nazo sifa zako, nitangaze pote } *2

  2. Uamkapo asubuhi ndugu yangu, umshukuru Mungu
    Kwa jinsi alivyokulinda usiku wenye giza tororo
    Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha
  3. Ufikapo safari yako ndugu yangu, umshukuru Mungu
    Kwa jinsi alivyokulinda na ajali za barabarani
    Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha
  4. Shikaneni mikono sasa yote muinyanyue juu
    Semeni kwa shangwe na mbwebwe maneno haya kwa furaha
    Ameweza Bwana Mungu kweli ameweza ameweza
  5. Akina mama simameni sasa mpige vigelegele
    Na kina Baba nyanyukeni mpige makofi ya shangwe
    Muimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha