Mbingu Zimenena

Mbingu Zimenena
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CategoryZaburi
ComposerJ. C. Shomaly
Views6,800

Mbingu Zimenena Lyrics

  1. { Mbingu zimenena, wokovu wa Mungu umekaribia,
    Nao wenye mwili watauona wokovu wa Mungu } *2
    Dondokeni enyi mbingu toka juu uu,
    Na mawingu yamumwage mwenye haki iii
    Na! Na! nchi ifunukefunuke
    bahari na iyumbeyumbe sasa
    { Miti nayo ichezecheze ichezecheze ichezecheze
    Milima iyumbeyumbe kwa furaha mbele za Mungu,
    Maana ametuokoa tumshangilie Mungu. } *2

  2. Nchi imekombolewa aa,
    Kwa kifo chake Mwokozi, Bwana hakika
  3. Watu wamekombolewa aa,
    Kwa kifo chake Mwokozi, Bwana hakika
  4. Wale wasioamini iii ii,
    Waamini waokoke, waache dhambi