Mbona Nahangaika Lyrics

MBONA NAHANGAIKA

@ D. Mdodo

{ Mbona nahangaika, mkiwa mimi,
Sina hata wa kunifuta machozi } *2
Ni aibu gani iliyonitanda,
Najuta hata siku ya kuzaliwa kwangu
{ Maskini mimi, nitakuwa mgeni wa nani,
Nakulilia e Mungu uniokoe } *2

 1. Taabu na matatizo yanisonga mimi
  Shida nazo karaha zanisumbua mimi,
  Mungu ufanye hima uniokoe.
 2. Nimeugua nikilalama, mnyonge mimi,
  Sina rafiki wala mtetezi, mkiwa mimi
  Wote wamenigeuka kuniwinda,
 3. Kila waliwazalo juu yangu ni baya,
  Kuugua kwangu kumbe ni furaha kwao
  Walitaka nife nisahaulike.
Mbona Nahangaika
COMPOSERD. Mdodo
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
MUSIC KEYD
TIME SIGNATURE3
8
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments