Moyo Wangu Unakutamani
| Moyo Wangu Unakutamani | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Tazameni Miujiza (Vol 2) |
| Category | Ekaristia (Eucharist) |
| Composer | Bernard Kiundi |
| Views | 11,465 |
Moyo Wangu Unakutamani Lyrics
{ Moyo wangu unakutamani,
Moyo wangu unakutamani Mungu wangu } *2
{ Kwa sauti nzuri mimi nikuimbie ee Mungu wangu,
Nitangaze sifa zako milele na hata milele } *2- Nikuambie nini Bwana, ujue ninakupenda
Moyo wangu umekuambia uso wako nitautafuta
Usinifiche uso wako ee Mungu Muumba wangu - Umenitendea mambo mengi, makubwa ya kushangaza
Sasa mimi nitazitangaza fadhili zako Bwana wangu
Asubuhi hata usiku ee Mungu nitakusifu - Nibariki ee Mungu wangu, siku zote za maisha yangu
Nikusifu wewe daima nitangaze uwezo wako
Usiwe mbali Mungu wangu naomba usiniache.