Mpigieni Bwana Lyrics

MPIGIENI BWANA

Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wacha Mungu,
Kusifu kwawapasa *2 (wenye) wenye moyo mnyofu

 1. Enyi watumishi wa Bwana lisifuni,
  lisifuni jina la Bwana
 2. Jina la Bwana litukuzwe,
  Sasa na hata milele
 3. Toka mawio ya jua na hata machweo yake
  Jina la Bwana lisifiwe
 4. Bwana ametukuka juu ya mataifa yote
  Utukufu wake wazipita mbingu
 5. Nani ni sawa na Bwana,
  Mungu wetu aketiye juu?
 6. Humwinua fukara kutoka mavumbini
  Na kumkweza maskini kutoka unyonge
Mpigieni Bwana
CHOIR
CATEGORYZaburi
 • Comments