Mshike Mshike

Mshike Mshike
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMshike Mshike (Vol 5)
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly
Views13,244

Mshike Mshike Lyrics

  1. { Hebu wanadamu na tufikirie sasa ni wapi tutakwenda,
    Vita vimezidi amani hakuna shetani ametia nanga } *2
    Mshike mshike kila kona watu wakimbilia usalama
    Lo! Lo! hili jambo limekuwa kawaida
    Ona wazee na watoto wateseka
    Mshike mshike, mshike mshike
    mshikeshike huu utaisha lini?
    (Tumuombe Mungu), atikise huu mshikemshike

  2. Ulimwengu wote umekuwa na visa vya ajabu,
    Pande moja vita pande nyingine mambo ya ajabu
    Tujisitiri wapi, kila pande machungu,
    Tunakuomba ee Mwenyezi utupe usalama Baba
  3. Watu nao wamekuwa wakali kuliko wanyama
    Tunaishi kama hakuna kizazi kingine tena
    Vita vya kila siku, uhasama wa mali,
    Kizazi chetu kimekuwa dhiki tena ukiwa sana
  4. Ulimwengu nao umekuwa jeneza la vijana,
    Kuvaa vibaya madawa makali wanatumia
    Eti wao wajanja, waenda na wakati
    Hawajui maisha yana mwisho silaha yao pombe
  5. Hebu fikiria unayefanya mambo haya yote,
    Ujue ya kuwa kila lenye mwanzo linao mwisho,
    Acha ya kidunia, faida ya ukiwa
    Mtegemee Mungu unayo nafasi hii kabla hujafa