Mshipi Lyrics

MSHIPI

@ E. F. Jissu

Ni nani aliye Mungu, Mungu ila Bwana
Ni nani aliye mwamba, mwamba ila Mungu
{Ni Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu aha!
Ni Mungu ndiye kimbilio la unyonge wangu aha!
Naye anaifanya kamilifu njia yangu } *2

 1. Ni yeye Bwana aliye nguvu zangu nampenda sana
  Ni yeye Jabali langu na boma langu na Mwokozi wangu
  Mungu wangu mwamba wangu ninayemkimbilia
  Ngao yangu na pembe ya wokovu wangu
  na ngome yangu
 2. Katika shida zangu nilimwita Bwana ee Bwana
  Na kumlalamikia Mungu ee Mungu
  Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake
  Kilio changu kikaingia masikioni mwake
 3. Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu
  Akanilipa sawasawa na haki yangu
 4. Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa
  Hivyo nitaokoka na adui zangu
Mshipi
COMPOSERE. F. Jissu
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMMSHIPI (VOL. 22)
CATEGORYZaburi
REFPs. 18
MUSIC KEYE Flat Major
TIME SIGNATURE3
8
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
NOTES Open PDF
 • Comments