Mshukuruni Mwokozi Lyrics

MSHUKURUNI MWOKOZI

@ Joseph Makoye

Mshukuruni Mwokozi enyi mataifa
Pigeni vigelegele pigeni makofi
Tangazeni rehema zake leo asubuhi
Semeni ya kuwa Bwana ni mwenye adili

  1. Njooni tumwimbie Bwana, mwamba wa wokovu wetu
    Mikononi mwake zimo bonde za dunia
    Bahari ni yake ndiye aliyeiumba
    Na mikono yake alituumba sisi
  2. Bwana ametamalaki mataifa watasema
    Ameketi juu ya makerubi mbinguni
    Yeye Bwana katika Sayuni ni mkuu
    Katukuka juu ya mataifa yote
  3. Mshangilieni Bwana mwimbieni na zaburi
    Vinanda na baragumu vyote mpigieni
    Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema
    Kwa kuwa fadhili zake ni za milele
Mshukuruni Mwokozi
COMPOSERJoseph Makoye
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE2
4
  • Comments