Msifuni Mungu Wenu
   
    
     
         
          
            Msifuni Mungu Wenu Lyrics
 
             
            
- Msifuni Mungu wenu enyi viumbe vyake
 Pazeni sauti zenu, mmwimbie kwa furaha
 {Leteni ngoma (leteni), leteni kinanda leteni na zeze
 Pia na midomo ifunguke vinywa vyenu vifunuke
 Tumsifu (tumsifu) tumsifu, tumsifu Bwana
 Tumsifu Mungu wetu aliyetuumba}
- Kusanyeni viumbe vyote viumbe vyote vya duniani
 Vimuimbie kwa shangwe, virukeruke mbele za Bwana
- Tumieni ulimi wenu kwa kuvipiga vigelegele
 Mmwimbie kwa shangwe mrukeruke mbele za Bwana
- Kila kiumbe duniani na kifungue kinywa chake
 Kishangilie kwa nguvu na kimuimbie kwa furaha