Mtunze Ndoa

Mtunze Ndoa
Performed bySt. Benedict Rapogi
AlbumHuyu Ni Yesu (Vol 1)
CategoryHarusi
ComposerJ. C. Shomaly
Views6,092

Mtunze Ndoa Lyrics

  1. Mungu amewaunganisha
    { Mtunze ndoa hii yenu (kwa mapendo)
    Mtunze ndoa hii yenu, mwanga wenu upendano } *2

  2. Mbele ya kanisa lake Mungu - mmeunganishwa ninyi
    Pendo na amani ziwe kwenu - ndoa itakate hima
  3. Mume umpende mke wako - iwe fumbo lako tuzo
    Mke umtunze mume wako - mbinguni katunukiwa.
  4. Vita na ugomvi vijitenge - omba radhi ukosapo
    Choyo na anasa visiwepo - mwanga wenu upendano
  5. Nyumba ya amani lengo lenu - Kristu tegemeo lenu
    Ndoa ni patano takatifu - timilifu kwake Mungu
  6. Mungu awajaze neema zake -m`barikiwe na watoto
    Msiwapoteze wana wenu - wote mali yake Mungu