Mungu Baba Pokea Lyrics

MUNGU BABA POKEA

@ Joseph Makoye

 1. Mungu Baba pokea sadaka yetu leo
  Tukutoleayo kwa jina la Mwanao
  Ya Abeli na Ibrahimu ilikupendeza
  Yetu Baba ipendeze ipokee

  Ipokee - sadaka yetu
  Ndilo fumbo - la kukupendeza
  La Baba na Mwana na Roho Mtakatifu *2
 2. Njooni wote tutoe sadaka yetu leo
  Kwa sifa na utukufu wake Mwenyezi
  Mkate huu na divai viwe mwili wake
  Kwa heshima kuu sadaka tumtolee
 3. Ee Mwenyezi tupokee tuwe mali yako
  Twakusihi kwa shukurani kuu tupokee
  Tunakutolea nguvu kazi na mavuno
  Kwa huruma yako dhambi tuondolee
 4. Kama mwanzo Mungu Baba a-si-fiwe
  Na mwanaye ndiye aliyetukomboa
  Roho Mtakatifu ndiye wetu mfariji
  Utatu Mtakatifu Mungu mmoja twakiri
Mungu Baba Pokea
ALT TITLEIpokee Sadaka Yetu
COMPOSERJoseph Makoye
CHOIRSt. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam
CATEGORYOffertory/Sadaka
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE2
4
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments