Nipokee Mungu wangu nipokee *2
Mbele yako ninakuja daima
Sinitupe mbali nawe, mimi mwenye dhambi
Nipokee Mungu wangu wangu nipokee
- Adui wako shetani amenizingira, na mitego ya kila aina
Nifanye nini Bwana nisipotee *2
- Kila jambo nifanyalo, laenda kombo Bwana
Sijiwezi bila msaada wako, nifanye nini Bwana nikufikie
- Mali yangu yote Bwana nitakurudishia
Mimi pia mali yako Bwana, nifanye nini Bwana unipokee
- Kwako Bwana nitadumu milele yote Bwana
Na daima nikutumikie, nifanye nini Bwana nifike kwako
|
|
|