Mwili wa Bwana Yesu Lyrics

MWILI WA BWANA YESU

@ F. A. Nyundo

 1. Mwili wa Bwana Yesu, chakula cha Mbingu
  Ni chakula cha roho, chenye uzima
  Hima uwe nasi ee Bwana Yesu
  Ukatushibishe chakula bora
  Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
 2. Yesu alituambia, Yeye ni chakula
  Ni chakula cha roho, chenye uzima
  Sote twaamini, ni mwili wake
  Pia twaamini ni damu yake
  Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
 3. Yesu alituambia, kuwa tumpokee
  Ni chakula cha roho, chenye uzima
  Ee Bwana mkombozi tunakuomba
  Kwa chakula hiki tuinamie
  Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
 4. Hii ndiyo karamu, aliyotuachia
  Ni chakula cha roho, chenye uzima
  Alaye mwili na kunywa damu
  Ana uzima wa siku zote
  Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
Mwili wa Bwana Yesu
COMPOSERF. A. Nyundo
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
MUSIC KEYA
TIME SIGNATURE3
8
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments