Nalifurahi Waliponiambia

Nalifurahi Waliponiambia
Performed by-
CategoryEntrance / Mwanzo
Views29,569

Nalifurahi Waliponiambia Lyrics

  1. Nalifurahi waliponiambia twende,
    Nyumbani mwa Bwana *2
    Miguu yetu (u yetu) imesimama
    Imesimama ndani ya malango yako, ee Yerusalemu

  2. Yerusalemu uliyojengwa,
    Kama mji ulioshikamana *2
  3. Huko ndiko walikopanda,
    Kabila za Bwana Mungu wetu*2
  4. Kwa ajili ya ndugu zetu
    Na rafiki amani iwe nawe *2
  5. Kwa ajili ya nyumba ya Bwana
    Nitafute mema siku zote*2