Nani ni Nani Lyrics

NANI NI NANI

@ R. Masanja

Nani ni nani, ni nani ni nani,
Ni nani ni nani, nani kama Mungu
Mwenye uwezo, na mwenye ukuu
Ni nani ni nani nani kama Mungu

 1. Ameniumba, jinsi nilivyo, nipendezavyo ni nani kama Mungu
  Niseme nini, niimbe nini, nilie vipi, ni nani kama Mungu
 2. Tazama jua, mwezi na nyota, mbingu na nchi . . .
  Nao usiku, jua li wapi, ni maajabu ni nani kama Mungu
 3. Ananilinda, mchana kutwa, pia usiku, ni nani kama Mungu
  Nikitembea, nikisimama, ananilinda , ni nani kama Mungu
 4. Tazama ndege wa msituni wanavyoishi , ni nani kama Mungu Hawana shamba wala vilenge anawalisha , ni nani kama Mungu
 5. Na maarifa, tuliyonayo, yeye katupa, ni nani kama Mungu
  Njooni pamoja, tumuimbie, na tumsifu, ni nani kama Mungu
Nani ni Nani
ALT TITLENi Nani Kama Mungu
COMPOSERR. Masanja
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMMSHIPI (VOL. 22)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments