Nasadiki (Misa Elizabeti)

Nasadiki (Misa Elizabeti)
Performed by-
CategoryTBA
Views3,128

Nasadiki (Misa Elizabeti) Lyrics

  • Ninasadiki kweli ninasadiki
    (kweli) ninasadiki *2


    Mungu Baba mwumba vyote, ninasadiki
    Na mwanawe Yesu Kristu,
    Mkombozi wa watu wote,
    Ni mzaliwa na Maria
  • Alikufa msalabani,
    Kwa ajili yetu sisi
    Siku ya tatu kafufuka,
    Alipaa mbinguni
  • Yuko kuume kwa Baba,
    Atakuja kuhukumu
    Naye roho mtakatifu,
    Ndiye mleta wa uzima
  • Na Kanisa Katoliki
    Takatifu la mitume
    Naungama ubatizo
    Ufufuko na uzima