Nasadiki (Misa Kariobangi)

Nasadiki (Misa Kariobangi)
Performed by-
CategoryTBA
Views16,500

Nasadiki (Misa Kariobangi) Lyrics

  • Nasadiki kwa Mungu mmoja - Ninasadiki
    Ndiye Baba yetu mwenyezi -
    Mwumba mbingu pia dunia -
    Nasadiki kwa Yesu Kristu -

    Nasadiki nasadiki - ninasadiki
    Nasadiki nasadiki - ninasadiki


    Mwana wa pekee wa Mungu -
    Mwenye kuzaliwa kwa Baba -
    Akapata mwili kwa Roho -
    Kazaliwa naye Bikira -
  • Kisha yeye kasulubiwa -
    Kwa amri ya Ponsio Pilato -
    Kwa ajili yetu kateswa -
    Akafa na akazikwa -
  • Kafufuka katika wafu -
    Kapaa juu Mbinguni -
    Ameketi kuume kwake -
    Mungu Baba yetu mwenyezi -
  • Ndipo atakapotokea -
    Kuhukumu wazima na wafu -
    Kwake Roho Mtakatifu -
    Kwa kanisa la Katoliki -
  • Ushirika wa watakatifu -
    Ondoleo la dhambi zetu -
    Nangojea ufufuko wa miili -
    Na uzima wa milele -