Nasadiki (Misa Taita)

Nasadiki (Misa Taita)
Performed by-
CategoryTBA
Views5,582

Nasadiki (Misa Taita) Lyrics

  1. Nasadiki kwa Mungu mmoja *2
    Mwumba mbingu na dunia *2
    Na kwa Bwana Yesu Kristu
    Mwana wake wa pekee

    Nasadiki kwa Mungu Baba -
    Nasadiki nasadiki Mungu aliyetuumba nasadiki nasadiki
    Na kwa mwana mkombozi -
    Na kwa roho wa uzima -

  2. Alitungwa kwa uwezo wake*2
    Roho mtakatifu *2
    Kazaliwa na Maria
    Yule mama na bikira
  3. Akateswa kwa Pilato ndipo *2
    Akasulubiwa *2
    Kafa tena akazikwa
    Akashuka kuzimu
  4. Siku ya tatu kafufuka, akapaa *2
    Hata mbinguni *2
    Amekaa kuume kwa Mungu
    Baba aliye Mwenyezi
  5. Atakuja kuhukumu wazima pia *2
    Na wafu *2
    Na ufalme utakuwa
    falme wake wa milele
  6. Nasadiki kwa kanisa takatifu*2
    Takatifu Katoliki Katoliki
    Shirika la watakatifu
    Maondoleo ya dhambi zetu

    Nangojea ufufuko wa miili*2
    Toka kwa wafu *2
    Na uzima wa milele
    Yote hayo nasadiki