Nasadiki Kwa Mungu (Mbingu na Dunia)

Nasadiki Kwa Mungu (Mbingu na Dunia)
Performed by-
CategoryTBA
Views5,174

Nasadiki Kwa Mungu (Mbingu na Dunia) Lyrics

  1. Nasadiki kwa Mungu mmoja, Mwumba Mbingu na dunia
    Na kwa Yesu Kristu mwanaye, Wa pekee Bwana wetu

    Nasadiki ninasadiki kweli ninasadiki
    Nasadiki kwa Mungu Mmoja

  2. Akapata mwili kwa tendo, Lake Roho Mtakatifu
    Kazaliwa naye Bikira, Akateswa kwa Ponsio Pilato
  3. Akasulubiwa akafa, Akazikwa kaburini
    Na kuzimu akashukia, Kafufuka siku ya tatu
  4. Akapaa juu Mbinguni, Ameketi kuume kwake
    Mungu Baba yetu Mwenyezi, Muumba Mbingu na dunia
  5. Ndipo atakapotokea, Kuhukumu wazima na wafu
    Na uzima wake milele, Utadumu bila mwisho
  6. Nasadiki kanisa ni moja, Ni kanisa takatifu
    Ni kanisa la Katoliki, Ni kanisa la mitume
  7. Ushirika wa watakatifu, Ondoleo la dhambi zetu
    Nangojea ufufuko wa mwili, Na uzima wa milele