[s/a] Ninatazama juu angani nikiomba msaada
Mateso yananizidi, hakuna anayekuja
Nafungua mikono yangu naleta sala yangu
Ee Bwana nisaidie, Mungu unihurumie
Navumilia tu mimi ninavumilia tu
(Bwana nateseka)
/s/
Navumilia tu, mimi ninavumilia tu,
Navumilia tu, kwani haya yote yana mwisho
Navumilia tu, mimi ninavumilia tu,
Navumilia tu, kwani ipo siku yatakwisha
/a2/
Navumilia tu, ninavumilia tu mimi
Navumilia tu, kwani haya yote yana mwisho
Navumilia tu, ninavumilia tu mimi
Navumilia tu, kwani ipo siku yatakwisha
/ t2 / a1 /
Bwana nateseka, unihurumie kwa uwezo wako
Naamini Bwana
Nipo kwenye shida, Bwana niokoe sikati tamaa,
Naamini Bwana, ipo siku yatakwisha
/t/
Navumilia tu mimi, ninavumilia tu
Navumilia tu, kwani haya yote yana mwisho
Navumilia tu mimi, ninavumilia tu
Navumilia tu, kwani ipo siku yatakwisha
/b/
Navumilia tu mimi, navumilia tu mimi
Navumilia tu, haya yote yana mwisho
Navumilia tu mimi, navumilia tu mimi
Navumilia tu, ipo siku yatakwisha
Nalia kwa uchungu, machozi yananitiririka,
Mateso ya dunia hii, naona yamekidhiri,
Huyu mwovu shetani hakika ananisonga sana
Ninakuomba ee Bwana unisaidie hima
Navumilia tu mimi ninavumilia tu
(Bwana nateseka)
Vitisho vya dunia, magonjwa dharau masengenyo
Na kunyanyasa wadogo, haya yote yatapita
Nangojea kwa hamu, Bwana utakapokuja tena
Nije niungane nawe, kwenye raha ya milele
Navumilia tu mimi ninavumilia tu
(Bwana nateseka)
Ewe mama Maria, naomba uniombee mama
Kwa Yesu mwanao mpenzi, ili aje aniokoe
Roho mtakatifu Mungu anipe ujasiri,
Hekima na pia nguvu, elimu pia uchaji
Navumilia tu mimi ninavumilia tu
(Bwana nateseka)
*Kwa wote walio katika taabu, uchungu na mateso ya aina yoyote; hasa WAGONJWA - ''Usikate tamaa, Mungu atasikia sala yako na atakufanyia miujiza. Ipo siku yatakwisha.''
Related Songs
Mwanadamu Kumbuka
Deo Kalolela - Mtoni Choir - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Maisha Yetu ni Mafupi
Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Maneno Saba ya Yesu Msalabani
E. Z. Ng - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Tulilikane Mathina Make Yesu
(traditional) - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Bwana Yesu Twakumbuka
Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Amin Amin Nawaambia
Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Watoto wa Mayahudi
Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Kristu Amekuwa Mtii
A Muyonga - St. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Yesu Akalia
G. A Chavalla - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Matumaini ya Safari
Marcus Mtinga - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Kisha Nikaona
Alfred Ossonga - St. Joseph Migori - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Kuteswa Kwake
Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Salamu Ee Msalaba
Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Huu Ndio Mti wa Msalaba
(traditional) - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Mbona Nahangaika
D. Mdodo - St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) - Kwaresma na Toba (Lent & Repentance)