Ndugu Kaza Mwendo Lyrics

NDUGU KAZA MWENDO

@ F. Mtegeta

Ndugu yangu kaza mwendo Safari bado ni ndefu
{Ina mabonde mengi pia na milima (mingi)
Ina wanyama wengi tena wa kutisha (sana)
Usilege'legee kaza mwendo tutafika.}*2

 1. Usali na kuomba ufike salama
  Kwa maana safari yetu ina vikwazo vingi
  Kuna mbwa mwitu wanaonyemelea roho za watu *2
 2. Tunza imani yako usiyumbeyumbe
  Tena usikate tamaa kumuabudu Muumba wako
  Parapanda itakapolia ikukute u tayari *2
 3. Ole wanafiki na wagombanishi
  Kwa sababu hukumu yaja kwa wasiopenda amani
  Watakuja lia na kusaka meno siku ya hukumu *2
Ndugu Kaza Mwendo
COMPOSERF. Mtegeta
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMMSHIPI (VOL. 22)
CATEGORYTafakari
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments