Ndugu Zangu Twendeni

Ndugu Zangu Twendeni
Performed by-
AlbumViuzeni Mlivyo Navyo
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerBasil Lukando
Views5,695

Ndugu Zangu Twendeni Lyrics

  1. Ndugu zangu twendeni - tukatoe sadaka
    Twende kwa moyo safi - tukatoe sadaka

    Kwani,
    Ukimpa Mungu wako sadaka kwa moyo mnyofu,
    Naye,
    Naye Mungu atakuwa na neema siku zote.

  2. Twende kwa ukarimu - tukatoe sadaka
    Mkate pia divai - tukatoe sadaka
  3. Mazao ya mashamba - tukatoe sadaka
    Hata na fedha zetu - tukatoe sadaka
  4. Hata kidogo twende - tukatoe sadaka
    Hata na nyoyo zetu - tukatoe sadaka