Ngoja Nicheze Lyrics

NGOJA NICHEZE

@ Bernard Mukasa

Tazama mimi ninavyopumua,
Tazama mimi nilivyo na nguvu *2
Hizo zote - ni neema bure toka kwa Mungu
Na mimi leo - ngoja nicheze muone,
Nitamsifu ngoja nicheze muone,
Bila kuchoka - ngoja nicheze muone aee

 1. Tazama mimi nakula na kushiba,
  Tazama mimi nalala nasinzia
  Tazama naamka mimi mwenyewe e,
  Tazama tazama ah tazama aa aha
 2. Tazama mimi naweza kuongea,
  Tazama mimi naimba bila shida
  Tazama naweza kucheza mwenyewe e
  Tazama tazama ah tazama aa aha
 3. Nikiugua ona napewa pole,
  ninapofiwa ndugu mwanifariji
  Tazama niwapo na shida wanajaa a
  Tazama tazama ah tazama aa aha
 4. Nikikosea huwa nasamehewa,
  Nikiudhiwa ndugu mwanitetea
  Tazama dhuluma haitaniua a
  Tazama tazama ah tazama aa aha
 5. Nikifurahi ndugu washerehekea,
  Nikiudhiwa ndugu wasononeka
  Tazama ninaishi kati ya watu u
  Tazama tazama ah tazama aa aha
 6. Na yote haya najaliwa na Mungu,
  Amenipenda upeo wa upendo
  Tazama na mimi nitamtukuza a
  Tazama tazama ah tazama aa aha
Ngoja Nicheze
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMungu Yule
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments