Ngong Ngong Lyrics

NGONG NGONG

@ Alfred Ossonga

[s:] Ngong ngong ninagonga ee Bwana nisikie
[w:] Nimo malangoni ninakuita
[s:] Ngong ngong ninagonga mlango wako Bwana
[w:] Bwana nipokee nikaribishe
[s:] Nasikia kwa Bwana kuna chakula
[w:] Nimekuja Bwana unishibishe
[s:] Nasikia ya kwamba kuna kinywaji
[w:] Nimekuja leo niburudike
[s:] Bwana unipokee nisikilize
[w:] Unipe neema unibariki

 1. Nyumba yake Bwana ni nyumba ya sala, endeni
  kwa heshima, tukaijongee meza ya mapendo, kwa furaha
 2. Nyumbani mwa Bwana mna neema nyingi nendeni
  mkapewe, tuugonge mlango wake pamoja, tuingie
 3. Bwana nimekuja leo na mapema, Mbele ya nyumba
  yako, unikaribishe hekaluni mwako, nakuomba
 4. Sala zangu na dua zangu natoa Bwana zikufikilie
  Unifungulie masikio yako siku zote
Ngong Ngong
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNitachezacheza
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments