Ni siku Tukufu

Ni siku Tukufu
Performed by-
CategoryPasaka (Easter)
Composer(traditional)
Views7,637

Ni siku Tukufu Lyrics

  1. Ni siku tukufu, aleluya amina
    Ya kupumzika, aleluya amina
    Tuache shughuli, tumwabudu Mungu
    Bwana wa Mbingui, aleluya amina.
  2. Ni siku tukufu, aleluya amina
    Tukufu kabisa, aleluya amina
    Njooni ndugu zangu, tumwabudu Mungu
    Na kwa roho wa kweli, aleluya amina
  3. Ni siku tukufu, aleluya amina
    Ya furaha mno, aleluya amina
    Yesu kafufuka na sasa yu hai
    Anatuombea, aleluya amina
  4. Ni siku tukufu, aleluya amina
    Ndiyo maarufu, aleluya amina
    Tunaye Mwokozi, atuongozaye
    Sasa na milele, aleluya amina