Niacheni Mimi Lyrics

NIACHENI MIMI

@ Alfred Ossonga

 1. Niacheni mimi niimbe nimwimbie Muumba wangu
  Niacheni mimi nicheze mbele zake Mwenye upendo

  Watu wote (leo) Nipisheni (mimi)
  Nimwonyeshe Bwana Mungu wangu jinsi ninavyompenda
  Nitaimba (mimi) nitacheza (sana)
  Nitarukaruka kwa furaha nikimsifu Mwenyezi
  Kwa nini nisiimbe(mimi), kwa nini nisicheze (mimi)
  Nami ninapoimba ninasali mara mbili
  Wanyama wanacheza wadudu wanarukaruka
  Wanamsifu Mungu wao siku zote kwa furaha

 2. Niacheni mimi niseme mbele zenu watu wa Mungu
  Niacheni niyatamke yaliyonijaa moyoni
 3. Niacheni niyaeleze maajabu ya Mungu wetu
  Niacheni niyaeleze aliyonitendea Mungu
 4. Niacheni niwaambie jinsi Bwana anipendavyo
  Niacheni nisimulie leo kesho hata milele
Niacheni Mimi
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNitachezacheza
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments