Nikupe Nini Mungu Wangu Lyrics

NIKUPE NINI MUNGU WANGU

@ Basil Lukando

{ Nikupe nini Mungu wangu, nikupe nini ee Mwokozi
Nikupe nini Bwana wangu cha kukupendeza } *2

 1. Kila nitakachoshika mbona bado ni kidogo
  Fadhili unazotenda kwangu mimi naogopa
  Ninakuomba Mwokozi, nifanyie msamaha na unipokee
  Mema unayoyatenda, nitafanya nini mimi nikurudishie
 2. Nakutolea mkate toka mmea wa ngano
  Nakutolea divai ni tunda la mzabibu
  Ninakuomba Mwokozi . . .
 3. Mchana hata siku wewe wanisimamia
  Na nikiwa safarini waniepusha ajali
  Ninakuomba Mwokozi . . .
 4. Nikiwa na matatizo Bwana hunisaidia
  Nikiwa kwenye majonzi Bwana unanifariji
  Ninakuomba Mwokozi . . .
 5. Kama njia sioni Bwana unaniongoza
  Na hata nikipotea kwako unanirudisha
  Nitatoa nini mimi, kitakachokuwa sawa na fadhili zako
  Nitaimba nini mimi, niyataje mema yote utendayo kwangu
Nikupe Nini Mungu Wangu
COMPOSERBasil Lukando
CATEGORYOffertory/Sadaka
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE6
8
SOURCETanzania
NOTES Open PDF


chakukupendeza


 • Comments